Mhe. Balozi na Watumishi wa Ubalozini

Salamu za mwaka 2023 kutoka Bodi ya Filamu Tanzania.

Bodi ya Filamu inatoa pongezi za dhati kwako na timu yako kwa kazi nzuri mnayoifanya katika kuiwakilisha inchi yetu kimataifa, hususani kwa kushirkiana na Bodi ya Filamu katika kuhudumia wageni wanaofika nchini kwa ajili ya kuandaa filamu.

Katika kuhakikisha kuwa Tanzania inavutia waandaaji wengi zaidi wa filamu kutumia mandhari na maudhui zilizopo Tanzania, Bodi imeandaa Makala fupi ya filamu inayolenga kuitangaza Tanzania kama eneo bora la uandaaji wa filamu. Tunaiomba ofisi yako isaidie katika kusambaza Makala husika kupitia tovuti na mitandao ya kijamii ya ofisi za ubalozi, na kwa wadau wapenzi wa nchi yetu. Makala husika inapatikana katika lugha ya Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa na Kihispania kupitia link zifuatazo: -

Tanzania The Prominent Filming Location - Swahili Version - YouTube

Tanzania The Prominent Filming Location - Spanish Version - YouTube

Tanzania The Prominent Filming Location - YouTube

Tanzania The Prominent Filming Location - French Version - YouTube

Tunashukuru sana kwa ushirikiano wako, na tutafurahi kuendelea kushirikiana zaidi katika masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya filamu.

Ninaomba kuwasilisha.