Ubalozi wa Tanzania Brussels, Ubelgiji unapenda kuwatangazia na kuwakumbusha watanzania kuhusu uwepo wa fursa za ufadhili wa masomo na utafiti zinazotolewa kwa Tanzania na Serikali ya Ubelgiji na Umoja wa Ulaya. Fursa hizi ni kwa ajili ya masomo kuanzia ngazi ya Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) Shahada ya Uzamili (Master Degree), Shahada ya Uzamivu (PhD) na utafiti (research). 

Fursa zilizopo kwa sasa ni kama ifuatavyo:

  1. VLIR-UOS Master Scholarship programme- inatoa fursa kwa wanafunzi kutoka nchi 29 duniani, ikiwemo Tanzania kwenda kusoma katika Taasisi za Elimu ya juu nchini Ubelgiji kwa ngazi ya shahada ya uzamili (Masters) katika eneo la Flenders. Kwa taarifa zaidi tembelea https://www.vliruos.be/en/scholarships

 

  1. VLIRUOS Short Initiative (SI) – inafadhili miradi ya utafiti katika taasisi za nchi mbalimbali zenye ubi ana VLIRUOS ikiwa ni pamoja na Tanzania. Kwa taarifa zaidi tembelea https://www.vliruos.be/en/scholarships

 

  1. ARES Scholarship Programme - inatoa ufadhili wa masomo nchini katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini Ubelgiji zilizopo katika eneo la Wallonia katika ngazi ya Shahada, Uzamili na Uzamivu. Ufadhili huu unatolewa kwa nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Tanzania. Kwa taarifa zaidi tembelea https://www.ares-ac.be/en

 

  1. Erasmus + Programme – Ni programme ya Umoja wa Ulaya inayotoa ufadhili wa masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu, utafiti na kubadilishana uzoefu miongoni mwa Taasisi za   elimu ya Juu. Fursa hii inatolewa kwa nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania. Kwa taarifa zaidi tembelea https://erasmus-plus.ec.europa.eu/

Nafasi hizi za masomo ni moja ya matunda ya mahusiano mazuri yanayotengenezwa kupitia diplomasia ya Tanzania. Hivyo ubalozi unatoa wito kwa watanzania kuchangamkia na kutumia fursa hizi ipasavyo kwa manufaa yao na ya Taifa. Kwa maaelezo zaidi unaweza kutembelea tovuti ya Ubalozi www.tzembassy.go.tz.