Katika eneo letu la uwakilishi kuna fursa mbalimbali zinazolenga kuendeleza sekta binafsi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Fursa hizo zinazotolewa na taasisi mbalimbali zilizopo katika eneo la uwakilishi ni pamoja na upatikanaji wa mikopo nafuu hususani kwa wajasiliamali wadogo. Baadhi ya taasisi zinazotoa fursa hizo ni pamoja na EDFI AgriFi, COLEACP ambazo zinaendelesha shuguli zao za kusaidia wajasiliamali wadogo ikiwa ni pamoja na utoaji mikopo chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya. Taarifa zaidi za namna ya kunufaika na fursa zinazotolewa na EDFI AgriFi na COLEACP zinapatikana kupitia: 

i. EDFI AgriFi: https://www.agrifi.eu/offer/apply-for-investment/ ; na

 ii. COLEACP:https://www.coleacp.org/current-programmes/fit-for-market-plus/ 

Vilevile, BIO ambayo ni taasisi ya fedha ya Ubelgiji ikijikita zaidi katika utoaji wa mikopo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa nchi zinazoendelea ikiwa ni pamoja na kusaidia wajasiliamali wadogo. Kupata taarifa zaidi kuhusu huduma zinazotolewa na taasisi hiyo tembelea https://www.bio-invest.be/. Ubalozi unatoa wito kwa wajasiliamali wa Tanzania kuchangamkia fursa hizi adhimu kwa kujitokeza kwa wingi na kuwasilisha maombi yao.