Tarehe 8 Desemba 2025 Balozi Jestas Abuok Nyamanga alikutana kwa mazungumzo na Bw. Geza Strammer, Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika katika Kurugenzi ya Ubia wa Kimataifa ya Umoja wa Ulaya ambapo walijadili masuala mbalimbali yenye maslahi ya pamoja katika ushirikiano baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya.

